Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza - Abdulwadh Sufiani, kijana mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa Lodge Lane mjini Liverpool, katika mahojiano na gazeti la Liverpool Echo alisema: "Kwa takriban miaka kumi sasa, kumekuwa na juhudi za kutuzuia tusifanye shughuli zetu, lakini Liverpool ina karibu Waislamu 40,000 ambao wengi wao hutegemea huduma zetu kwa ajili ya maziko. Tumewahi pia kupokea waombolezaji kutoka miji na maeneo ya mbali kabisa."
Akaendelea kusema: "Kwa masikitiko makubwa, hatupati msaada unaolingana na mahitaji yetu halisi. Ingawa idadi ya Waislamu ni kubwa sana, lakini sehemu yetu ya kuhifadhi na kuoshea maiti ina uwezo wa kuhudumia maiti mmoja tu kwa wakati mmoja."
Na akahitimisha kwa kusema: "Kilicho wazi kwa sasa ni kwamba tunakabiliwa na uhitaji mkubwa wa rasilimali na vifaa, ambavyo haviendani kabisa na idadi ya watu wanaohitaji huduma hizi."
Maoni yako